22 Desemba 2025 - 20:09
Walowezi wa Kizayuni kuuvamia Msikiti wa Al-Aqsa

Walowezi wa Kizayuni leo asubuhi, siku ya Jumatatu, kwa ulinzi na msaada wa majeshi ya uvamizi wa Israel, waliuvamia ua wa Msikiti wa Al-Aqsa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-  walowezi leo asubuhi, siku ya Jumatatu, kwa ulinzi wa majeshi ya uvamizi ya Israel, walivamia eneo la Msikiti wa Al-Aqsa.

Vyanzo vya ndani vimeripoti kuwa makumi ya walowezi waliuvamia msikiti huo na, chini ya ulinzi wa majeshi ya uvamizi, wakafanya ibada na taratibu za kichochezi za Kitalmudi.

Walowezi hao pia walifanya kile wanachokiita “sajda ya kishujaa” katika nyua za Msikiti wa Al-Aqsa, sambamba na siku ya nane na ya mwisho ya sikukuu ya Kiyahudi ya Hanukkah.

Inafaa kutajwa kuwa katika siku nane zilizopita, maelfu ya walowezi wamevamia eneo la Msikiti wa Al-Aqsa, kufuatia wito wa makundi ya walowezi wa Kizayuni wa kuongezwa mashambulizi dhidi ya msikiti huo na kuandaliwa maandamano ya kichochezi katika Mji wa Kale wa Quds (Yerusalemu).

Walowezi wa Kizayuni kuuvamia Msikiti wa Al-Aqsa

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha